SA国际传媒

Tafuta

2024.10.04  Bwana Sadyr Zhaparov, Rais wa Jamhuri ya Kyrgyzstan. 2024.10.04 Bwana Sadyr Zhaparov, Rais wa Jamhuri ya Kyrgyzstan.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa akutana na Bw.Sadyr Zhaparov,Rais wa Kyrgyzstan

Nchi ambayo kijiografia inakumbukwa Njia ya Hariri,iliyoko kati ya milima ya Tien Shan.Na ukumbusho wa misaada ya Kyrgyzstan iliwasili Vatican kati ya zawadi ambazo rais wa Jamhuri ya Asia,Bwana Sadyr Zhaparov alitaka kumpatia Papa wakati wa Mkutano wao tarehe 4 Oktoba 2024 mjini Vatican.

SA国际传媒

Papa Francisko na Rais Sadyr Zhaparov,Rais wa Kyrgyzstan Ijumaa tarehe 4 Okotba 2024 walikutana mapema asubuhi kwa takriban dakika 20, mjini Vatican kisha kwa mujibu wa itifaki mkutano wa rais uliendelea katika Sekretarieti ya  Vatican na Kardinali Pietro Parolin akiwa na  Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa  Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa.

Papa akiwa na mgeni wake, Rais wa Jamhuri ya Kyrgyzstan
Papa akiwa na mgeni wake, Rais wa Jamhuri ya Kyrgyzstan

Wakati wa mazungumzo yao yalikuwa mazuri kama ilivyo wasilishwa na  Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican kwamba “mahusiano mazuri kati ya Vatican na Kyrgyzstan yaliakisiwa hasa juu ya ushirikiano wa pamoja katika nyanja za afya, elimu na kiutamaduni na katika nyanja kadhaa za maisha ya Kanisa mahalia.” Kisha kulikuwa na "mabadilishano ya maoni juu ya mambo ya sasa ya kimataifa, kwa kuzingatia migogoro inayoendelea na masuala ya kibinadamu, kuonesha umuhimu wa kujitolea kwa haraka kwa kukuza amani.”

Rais wa Kyrgyzstan akiwa na Kardinali Parolin na Gallagher.
Rais wa Kyrgyzstan akiwa na Kardinali Parolin na Gallagher.

Zawadi

Mbali na mapambo ya kiasili  yaliyotengenezwa  kiikolojia katika milima ya nchi hiyo, Rais Zhaparov alimpatia Papa mchoro unaoonesha Basilika ya Mtakatifu Petro iliyotengenezwa kwa pamba za rangi na huduma ya chai iliyotengezwa kwa  ufundi, wa fedha kutoka katika migodi ya ndani.

Wakati wa kubadilishana zawadi
Wakati wa kubadilishana zawadi

Papa Francisko alijibu kwa kutoa  sanamu yaudongo yenye kichwa "Upendo na Huruma," nakala ya kitabu cha picha kwenye Jumba la Kitume na kilichokuwa na ujumbe wa amani wa mwaka huu 2024.

04 October 2024, 17:23